Serikali kuu kwa ushirikiano na muungano wa Jumuiya ya ulaya EU, inalenga kuhamisha asilimia 50 ya usafirishaji wa bidhaa za maua mboga na matunda kutoka usafiri wa ndege hadi usafiri wa baharini katika miaka 10 ijayo.

Hatua hii inatarajiwa kupunguza gharama ya usafirishaji wa bidhaa za mashambani kutumia ndege.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo katika bandari ya Mombasa gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amesema hapo awali kumeshuhudiwa kushuka kwa asilimia 25 hadi 30 ya bidhaa zinazosafirishwa kupitia angani huku akitaja gharama ya kusafirisha bidhaa kupitia kwa njia ya baharini kuwa rahisi na nafuu zaidi ikilinganishwa na njia ya Angani.

Nassir ameitaka serikali kuu kupitia bandari ya Mombasa KPA kutenga eneo maalum katika bandari ya Mombasa ambapo bidhaa zenye kuharibika kwa urahisi zinahifadhiwa.

Nassir amepigia upatu mpango huo wa kusafirisha bidhaa za mashambani kupitia bahari akisema utasaidia pakubwa katika kukua kwa uchumi wa kaunti na hata wa taifa zima kwa ujumla.


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo