Serikali ya kaunti ya Mombasa imerekodi ongezeko la asilimia 14 katika ukusanyaji wa mapato.

Haya yamedokezwa na gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir.

Kulingana na gavana Nassir ni kuwa ukusanyaji huo umeafikia na kupita matarajio yao.

Nassir aidha amesema kuwa sasa analenga kutia sahihi agizo la kisheria yaani Executive Order ili kuja na mfumo mpya wa ukusanyaji ushuru wa Mombasa ili kuimarisha zaidi ukusanyaji wa mapato ya kaunti.

Ameyasema haya katika mkutano uliowaleta pamoja wadau katika idara ya ukusanyaji ushuru kaunti ya Mombasa katika ukumbi wa Tononoka hapa Mombasa.