Wakulima katika kaunti ya Lamu wamehimizwa kutumia maghala yaliyojengwa na serikali kwa ajili ya kuhifadhi mazao yao.
Gavana wa kaunti ya Lamu Issa Timamy amesema kaunti hiyo iko na maghala manne ambayo yalijengwa kwa ajili ya wakulima na hakuna anayetumia maghala hayo.
Amesema kutokana na mvua inyavyoendelea kunyesha kuna matumaini ya watu kupata mavuno mazuri mwaka huu hivyo basi mazao hayo yanapaswa kuhifadhiwa vyema kabla ya kuuzwa.
Timamy ametoa wito kwa wakulima kuhifadhi mazao yao katika maghala ya serikali ili kuepuka hasara ya mazao hayo kuharibika au kununuliwa kwa bei duni kwani baadhi ya wafanyibiashara huwanyanyasa wakulima kwa kuwanunulia mazazo yao kwa bei ya chini sana.
Aidha amesema bajeti ya kilimo ya mwaka ujao itaongezwa ili kuboresha zaidi kilimo katika kaunti hiyo na kuongeza kiwango cha uzalishaji wa chakula kwa ajili ya wakaazi wa Lamu na hata kwa ajili ya biashara.


 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani