Sekta ya utalii kaunti ya Kilifi imetajwa kusambaratika pakubwa licha ya serikali ya kaunti hiyo kuunda mikakati ya kuiimarisha.

Viongozi wa sekta hiyo katika eneo la Malindi wakiongozwa na Francis Yeri,wamesema kuwa mahoteli mengi yamesambaratika jambo ambalo limelemaza sekta hiyo.

Kulingana na Yeri,idadi ya watalii wanaozuru Malindi,Watamu,Ngomeni na Kilifi imeshuka pakubwa.

Naye gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Mungaro amesema kuwa mikakati Zaidi inaendelezwa na serikali hiyo na serikali kuu ili uwanja wa ndege wa kimataifa wa malindi uweze kupanuliwa vyema.

Kulingana na Mungaro uwanja huo wa ndege utawezesha watalii kutoka nchi za nje kuja moja kwa moja hadi Malindi hali akisema kuwa ni hatua mojawapo yakuimarisha sekta hiyo.