Biashara ya mabuibui ya mitumba inaonekana kushika kasi katika kaunti ya Mombasa.

Bei ya chini ya mabuibui hayo ndio imetajwa kuwa sababu kuu ya biashra hio kunawiri.

Buibui moja la mtumba linauzwa kwa shilingi elfu moja ikilinganishwa na buibui jipya ambalo bei uwa zaidi ya shilingi 2,500.

Bonface Musyoka ni mfanyibiashara wa mabuibui ya mitumba katika eneo la Bombolulu ametaja kupata faida kubwa kutokana na biashara hio.

Ametaja kuwa biashara hio unoga zaidi wakati wa Ramadhani na sherehe za Eid ambapo wanunuzi wengi ujitokeza na kununua mabuibui kwa wingi.

Bonface anasema changamoto kuu wanayokumbana nayo ni utozwaji ushuru mkubwa.

Kwa upande wake Mteja kwa jina Fatma Omar ametaja mabuibui ya mitumba kuwa mazuri mno na yenye bei nafuu ikilinganishwa na yale mapya.Ametaja kuwa mara nyingi yeye ununua mabuibui ya mitumba.

Mwandishi:Haifa Mohammed