Takribani vijana 600 kaunti ya Mombasa watapata mafunzo ya uendeshaji bodaboda.

Haya ni kwa mjibu wa mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir.Akizungumza kwenye kikao na viongozi mbali mbali katika sekta ya Bodaboda hapa Mombasa Nassir amesema tayari ameweka mikakati kuhakikisha kuwa vijana kupitia ufadhili wake wanapitia mafunzo hayo ili kuwasaidia kujitaftia riziki.

Nassir amewaomba kila mwenyekiti wa kila gatuzi dogo, kaunti ya Mombasa kuorodhesha vijana 100 ili wapate mafunzo hayo kuanzi wiki hii.