Serikali kuu kupitia wizara ya Elimu imehimizwa kuanzisha mafunzo ya uzimaji moto shuleni kama njia mojawapo ya kukabili majanga ya moto yanapotokea shuleni.

Afisa mkuu wa dharura kaunti ya Mombasa Mohammed Basafar amesema hatua hiyo itasaidia kuimarisha usalama mashuleni.

Vile vile, Basafar amesema kupitia kwa mafunzo hayo wanafunzi watajengewa uwezo wa kutambua hatari za moto, kutumia vifaa vya kuzimia moto kwa usahihi na kuchukua hatua za haraka katika kudhibiti majanga kama hayo.

Basafar ameongeza kuwa kuna haja ya viongozi wa shule wakishirikiana na wizara ya Elimu kuweka mazingira bora kwa wanafunzi ili kuzuia visa vya moto mashuleni.

Aidha ameongeza kwamba kwa kushirikiana, viongozi wa shule wanaweza kuhakikisha kuwa miundombinu ya kuzimia moto iko salama na inapatikana kwa urahisi, pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini na kutatua mapema matatizo yanayoweza kusababisha majanga ya moto.

 


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo