Kiongozi wa chama cha DAP-K Eugene Wamalwa amekosoa hatua ya serikali ya kuongeza ushuru bila kujali mwananchi.

Akizungumza baada ya kukutana na gavana wa kaunti ya Mombasa, Wamalwa amesema kuwa wakenya wanazidi kuumia kutokana na sera za serikali kuhusu uchumi.

Wamalwa amekosoa baadhi ya viongozi wa muungano wa Kenya Kwanza wanaosema kuwa uchumi umeimarika.

Waziri huyo wa zamani wa ulinzi amesema kwamba muungano wa Azimio utaendelea kutetea maslahi ya wakenya dhidi gharama ya juu ya maisha.

Aidha, ameionya serikali ya Kenya Kwanza kuhusu kile alicho kitaja kuwa ina mpango wa kuchagua makamishna wa wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.

 


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo