Mahakama ya Mombasa imewapa polisi siku 21 kuwachunguza wanaume wawili wanaoshukiwa kuwasajili vijana kujiunga na makundi ya kigaidi katika taifa la Somalia na DRC.
Afisa mpelelezi amemwambia hakimu David Odhiambo kwamba Hussein Yusuf Mrafi na Ali Mwalimu Mwinyi wanashukiwa kuwa wanaajiri watu kuingia ISIS na Al Shabaab.
Wanashukiwa kutenda kosa la Kuajiri Wanachama wa Kundi la Kigaidi kinyume na Kifungu cha 13 cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi nambari 30 ya mwaka 2012.
Maafisa wa upelelezi wanaamini kuwa Mrafi, 27, na Mwinyi, 21, wanaweza kuwa sehemu ya kundi la magaidi katika eneobunge la Likoni, hapa Mombasa linalowasajili vijana kujiunga na magaidi wa ISIS na Al Shabaab katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Somalia.
Afisa wa upelelezi ameiambia mahakama kuwa alihitaji siku 30 kukamilisha upelelezi ikiwa ni pamoja na kuchukua simu tatu zilizokamatwa kutoka kwa mshukiwa wa kwanza kwa uchunguzi wa kitaalamu.
Katika hukumu yake hakimu Odhiambo alimpa mpelelezi siku 21 kukamilisha uchunguzi wake akiagiza kesi hiyo isikizwe tarehe 7 Mei 2024.


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo