Seneta mteule wa chama cha UDA hapa Mombasa Miraj Abdillah ametaka wakenya kutomnyoshea kidole cha lawama waziri wa Afya Susan Nakhumicha kuhusiana na mkwamo uliopo katika sekta ya afya humu nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari Miraj amesema kuwa waziri Nakhumicha hapaswi kulaumiwa kwani mzigo alioupata katika wizara hio ni mkubwa na anapaswa

kupewa muda kutekeleza majukumu yake.
Seneta huyo ameonyesha kusikitishwa kwake namna swala hili linavyoshughulikiwa na baadhi ya wakenya ikizingatiwa kuwa waziri wa afya ni wa jinsia ya kike.

"Hata sahi tunazungumzia masuala ya mbolea ambayo ni ghushi lakini vile vidole vya lawama vimeelekezwa kwa waziri ni vichache sana. Kwa nini sisi tumekuwa tukujirejelea kuonea jinsia ya kike? Mahali kokote ambapo mwanamke amepewa majukumu ndiko mahali ambapo sisi tunaonyesha udhaifu" Akasema Miraj.

Miraj amesema mkataba wa makubaliano CBA, kati ya serikali na madaktari ulifanyika wakati wa utawala uliopita hivyo basi hivyo basi wanafaa kuwa na subra.
Aidha Miraj ameongeza kuwa madaktari wanafaa kupatia serikali muda wa kulainisha masuala iliyorithi kutoka kwa serikali iliyopita.
Vile vile amewataka madaktari kuwa na utu kwani wakenya walala hoi ndio wanaotaabika wakati wanapoendeleza mgomo.

"Tunatatizika sana na madaktari kutokuwa katika sehemu zao za kazi ikifahamika kwamba wananchi ndio wanaoumia. Nyinyi ni wafanyikazi lakini sio wafanyikazi wa kawaida. Nyinyi ni kama mitume" Akaongeza Miraj.


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo