Zaidi ya wazee na watu wenye ulemavu milioni moja chini ya mpango wa Inua Jamii Cash Transfer wanatazamiwa kupokea Sh bilioni 8.9 kutoka serikalini ili kuwaepusha na hali ngumu ya kiuchumi iliyopo.

Waziri wa Utumishi wa Umma na Mipango Maalum Margaret Kobia aesema malipo hayo yatawekwa kwenye akaunti za walengwa waliosajiliwa kuanzia leo Jumatatu.

Kobia alisema kila mmoja atapokea Sh 8,000 ikiwa ni malipo ya miezi ya Machi, Aprili, Mei na Juni 2022.

Taarifa hiyo ilibainisha zaidi kwamba waliojiandikisha chini ya mpango wa NICHE, watapokea kiasi cha ziada cha hadi Sh4,000 kwa kila nyumba.


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo