Visa vya ulanguzi wa binadamu vimetajwa kukithiri katika mpaka wa Kenya na Tanzania huko Lungalunga kaunti ya Kwale.

Haya ni kulingana na shirika la kijamii la Peace Tree Network linalosema kuwa raia wa kigeni kutoka mataifa ya Somalia, Ethiopia na Tanzania ndio wanaosafirishwa kupitia mpaka huo.

Afisa wa shirika hilo Martha Okumu amesema kwamba shirika hilo limeanza kutoa mafunzo kwa mawakili wa nyanjani ili kukabiliana na visa hivyo.

Kwa upande wake wakili katika shirika la kituo cha sheria Zedekiah Adika amesema kuwa mafunzo hayo yataongeza viwango vya masomo ya mawakili hao.

Adika sasa anaitaka serikali kuwatambua mawakili hao ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika jamii.

 


 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani