Takribani wangonjwa 46 waliokuwa wameshindwa kugharamikia deni la matibabu yao katika Hospitali kuu ya Ukanda wa pwani wameruhusiwa kuondoka baada mgombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir kugharamikia madeni yao.

Wagonjwa hao waliokuwa wakihudumiwa katika Hospitali hiyo kwa maradhi tofauti tofauti walishindwa kulipia madeni yao licha ya wao kupona.

Benedicta Mbithe mkaazi wa Tudor ni miongoni mwao Anasema mwanawe mwanawe mchanga alikuwa amemea Jipu tumboni na kwamba haikuwa rahisi kwake kulipia matibabu ya mwanawe ikizingatiwa kuwa alikuwa hana uwezo wakugharamia matibabu yaliyomgharimu shilingi elfu 22.

Hata hivyo ametoa shukran kwa mjumbe huyo kwani alikuwa amepoteza matumaini ya kumtoa mwanawe ambaye alikuwa amelazwa Hospitalini humo kwa matibabu.

Kwa upande wake Mwalimu Bakari mkaazi wa eneo bunge la Likoni ambaye pia alikuwa miongoni mwa wagonjwa walioruhusiwa kuondoka,

Bakari alikuwa anaugua maradhi ya Saratani ya Jicho ameeleza afueni kwani alikuwa amefanyiwa oparesheni ila changamoto za kugharamikia huduma za matibabu ya maradhi hayo kwake ilikuwa kizungumkuti.

Haya yanajiri huku takribani shilingi milioni 1.8 zikitolewa kugharamikia madeni ya wagonjwa hao 46 waliohudumiwa katika Hospitali hiyo ya Makadara kwa maradhi mbali mbali.