Gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ameitaka idara usalama kaunti ya Mombasa kufichua wale wanao jihusisha na ulangulizi wa dawa za kulevya Mombasa.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupambana na ulanguzi wa mihadharati inchini gavana Nassir ameitaka idara ya usalama kuchapisha orodha ya walanguzi ambao idara hio imewakamata.

Kulingana na gavana Nassir wakaazi wa kaunti ya Mombasa wamekufa imani kwa kile anachosema kuwa janga la mihadharati ni la muda mrefu akisema kukamatwa kwa wanunuzi sio suluhu mwafaka la tatizo hilo.

Nassir ameitaka hatua ya haraka kuchukuliwa dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya Mombasa.

Kwa upande wake naibu wa gavana Francis Thoya ameitaja mradi wa kazi kwa vijana wa Mombasa yangu umesaidia pakubwa kupunguza idadi ya vijana kujiunga na makundi ya uhalifu.
Kulingana naye njia mwafaka ya kuwaepusha vijana na utumizi wa dawa za kulevya ni ajira.