Wanasiasa wametajwa kuchangia kwa kiwango fulani katika kuleta migawanyiko miongoni mwa wanajamii katika kaunti ya Lamu.

Imamu wa msikiti wa Jamiah eneo la Mokowe na ambaye ni mwanaharakati wa maswala ya amani Mohamed Bwanamku amesema mara nyingi wanasiasa huwagawanya watu katika msingi ya kikabila na dini hasa wanapotaka kufanikisha malengo yao ya kisiasa.

Amesema ipo haja ya viongozi wa kisiasa kushirirkiana na wale wa serikali ili kuleta uwiano katika jamii badala ya kueneza chuki.Ameongeza kuwa viongozi wanapaswa kuangazia zaidi masilahi ya umma badala ya kuweka mbele mambo yao ya kibinafsi.
Aidha amesema viongozi wa kidini pia wako na jukumu la kuleta jamii pamoja kwa kuhubiri mafunzo sashihi badala ya kupotoshha watu na mafunzo ya itikadi kali.

Haya yanajiri baada ya Watu watano kuuwawa katika vijiji vya Salama na Juhudi na nyumba zao kuchomwa moto na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al-Shabab katika kaunti ya Lamu.

Kulingana na taarifa kutoka kwa idara ya polisi watu takriban 30 waliokuwa wamejihami kwa bunduki, mapanga na visu wamevamia vijiji hivyo mwendo wa saa moja na nusu kuamkia leo na kutekeleza mauwaji hayo.

Kulingana na idara ya polisi watano waliouwawa ni Samuel Chomba Gacurai wa umri wa miaka 60, Reuben Mwangi Nyamu wa miaka 33,Peter Mureithi Githinji mwenye miaka 40,Mwenda Alias wa miaka 38 na Barrack Hussein wa mika 19 na ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya upili ya Bakanja.

Watano hao walifungwa kamba za miguu na mikono kabla ya kuchinjwa nje ya nyumba zao huku nyamba zao zikichomwa moto pamoja na mali zao.Mbali na kutekeleza mauwaji wavamizi hao pia wameiba mbuzi ,kuku, pesa takriban elfu 60 na vitu vyengine vya thamani kama vile simu za mkononi.Hata hivyo lengo la mashambulizi hayo halijabainika huku msako dhidi ya wauwaji hao ukiwa tayari umeanzishwa.