Serikali ya kaunti ya Lamu imefanikiwa kurudisha katika mikono ya serikali vipande vya aridhi zaidi ya 66 ambazo zilikuwa zimenyakuliwa na watu binafsi.

Waziri wa aridhi katika kaunti ya Lamu Tashirifa Mohamed amesema tayari serikali imetoa hatimiliki ya aridhi hizo ili kuzuia wanyakuzi kuzivamia tena.

Amesema nyingi ya aridhi zilizokuwa zimevamiwa ni aridhi za shule ,mahakama hospitali na hata makaburi ya umma huku akisisitiza kuwa serikali itandelea kufuatilia aziridhi zote za umma na kuzirudisha katika mikono ya serikali.

Ametoa onyo kwa wale wanaokalia aridhi za umma kinyume cha sheria kutoka kwenye aridhi hizo kabla ya kuchukuliwa hatua za sheria.

Aidha ametoa wito kwa serikali ya kitaifa kushirikiana na ile ya kaunti ili kufanisha vita dhidi ya unyakuzi wa aridhi katika kaunti hiyo.


 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani