Chama cha kisiasa cha PAA yaani Pamoja African Alliance kinachoongozwa na gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi kimepata pigo baada ya mwakilishi wa wadi ya mwawesa eneo la Rabai kukihama chama hicho.

Caro Cheupe ambaye amekuwa msitari wa mbele kupigia upatu chama hicho amehamia chama cha Jubilee kwa kile alichodai kuwa chama cha PAA kinataka kumpa tiketi ya moja kwa moja mpinzani wake Kenga Mpe.

Kulingana na Cheupe anaendelea kushauriana na wananchi katika eneo la Rabai katika azma yake ya kuwania kiti cha ubunge katika eneo hilo.

Hapo awali gavana Kingi aliahidi kuwa chaguzi za mchujo katika eneo hilo la Rabai zitakuwa za wazi na haki.

Wachanganuzi wa maswala ya kisiasa katika kaunti ya Kilifi akiwemo Anthony Kingi amesema kuwa migawanyiko ya kisiasa itaendelea kuonekana kwa wiki mbili zijazo.

Kuhama kwake kunajiri siku kadhaa kabla ya kufanyika kwa mchujo wa vyama huku gavana Kingi akiendelea na mipango ya kuimarisha chama hicho.