Serikali ya kitaifa imetakiwa kuweka usawa inapohudumia sekta za uvuvi na ukulima katika kaunti ya Lamu.

Hii ni baada ya kuonekana kuwepo kwa upendeleo katika baadhi ya sekta.

Mwenyekiti wa masuala ya uwiano wa kidini kaunti ya Lamu Mohammed Abdulkadir amesema serikali inaonekana kupendelea zaidi sekta ya ukulima kuliko ile ya uvuvi.

Abdulkadir amesema hii ni licha ya kuwa sekta zote hizo zinachangia pakubwa katika uchumi wa kaunti ya Lamu na taifa kwa jumla.

Amesema sekta ya uvuvi imewekewa vikwazo vingi ikilinganishwa na wakulima.Aidha amesema katika suala la ulipwaji wa ridhaa wakulima walilipwa kitambo baada ya kuchukuliwa mashamba yao kwa ajili ya ujenzi wa bandari huku wavuvi wakiwa bado hawajalipwa na maeneo yao ya uvuvi yaliharibiwa.

Amesema hii huenda ikaleta chuki baina ya jamii za wavuvi dhidi ya wakulima jambo ambalo linaweza kuhujumu amani hivyo basi ametoa wito kwa serikali kuweka usawa na kuhakikisha wavuvi wanapata haki zao.

 


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo