Mwaniaji wa kiti cha ubunge cha Mvita Said Mohammed Twaha ameendelea kuwahimiza wakaazi wa kaunti ya Mombasa kuchagua viongozi kwa misingi ya maendeleo badala ya kuzingatia mirengo ya kisiasa.

Twaha ambaye anawania wadhfa huo kwa tiketi ya chama cha Pamoja African Alliance (PAA) amesema kwamba chama ni mfano wa chombo cha usafiri ila zaidi watu wanafaa kuzingatia utendakazi na ajenda za mwaniaji yeyote badala ya kuzingatia chama au mirengo ya kisiasa.

Akizungumza kwenye hafla ya kufthuru akiwa pamoja na maimamu, maustadhi na maustadha kutoka maeneo tofauti ya kaunti ya Mombasa, Twaha amesema kwamba alijiunga na chama hicho kutokana na kwamba kinajali maslahi ya mpwani pamoja na kwamba kinapeana uhuru wa mtu kutoa maoni yake.

Ni kwenye hafla hiyo ambapo mgombea huyo wa ubunge ameahidi kushirikiana na viongozi wa dini zote kuhakikisha kwamba wao pia wanatambulika ipasavyo kwenye jamii ikiwemo kupeleka mswada katika bunge la kitaifa kuhakikisha kwamba walimu wa dini wanatambuliwa na tume kuwaajiri walimu nchini TSC.

Mwandishi- Ibrahim Juma Mudibo.


 

More Stories

Buriani jenerali Francis Ogolla

Idara ya polisi yasema mgomo wa madaktari ni usumbufu

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo