Tong-il Moo-Do ni mchezo unaoenziwa sana na mataifa ya bara Asia huku ukianza kupata mizizi katika mataifa mengine barani Afrika.

Mojawapo ya mataifa hayo ni Kenya.

Baadhi ya watu hutumia mchezo huo kama nji ya burudani huku sheria zake na zile za taekwondo na Judo zikiwa hazijaachana mbali.

Kunao wale walioenda hatua moja Zaidi na kutumia Tong-il Moo-Do kama njia ya kujihami.

Kaunti ya Taita Taveta ni miongoni mwa kaunti za Pwani zinazoshuhudia visa vya unyanyasaji wa kijinsia na kimapenzi.

Tarehe 21 mwezi Julai mwaka huu, kaunti hio ilizindua sera za kupambana na dhulma hizo na kuwa kaunti ya pili humu nchini kufanya hivyo baada ya kaunti ya Meru.

Hezron Mwabili ni mkufunzi wa Tong-il Moo-Do na anaamini kuwa hatua yake ya kuwafunza wasichana namna ya kujihami kutawasaidia pakubwa.

Mwabili anafunza wasichana wenye umri wa kati ya miaka 8 hadi 15 kwani kulingana nae, wao ndio walio katika hatari zaidi ya kudhulumiwa.

Anasema lengo lake ni kuona jamii yenye usawa na haki.

Mary Mwazighe ni mzazi na mwalimu katika shule ya upili ya upili ya Kombolio, wadi ya Bura, eneo bunge la Mwatate, kaunti ya Taita Taveta.

Mwazighe ana mtoto anaefanya tae kwondo na anasema wasichana kupewa mafunzo hayo kutawasaidia kuzingatia mno masomo yao.

Vile vile amewahimiza wazazi wengine kuwaruhusu watoto wao wa kike kupata mafunzo hayo ya kujihami ili kupunguza dhulma za kijinsia.

Baadhi ya wasicha wanaofunzwa na Mwabili niliozungumza nao ambao hawakutaka sauti zao zirekodiwe, wamesema kupitia mafunzo wanayopata, ujasiri wao umeimarika kwa kiwango kikubwa.

Mwabili anasema anatazamia kupata vifaa zaidi ili kuongeza idadi ya wale anaowafunza kwa sasa kwani zipo changamoto anazokumbana nazo zinazoohusu fedha.

Kufikia hapo ndipo ninapotamatisha Makala haya ya Tonge la Kujihami nimekuwa wako mtayarishi na msimulizi, jina langu ni Oscar Ochieng’.

 

Page 4 of 4
Show more post

 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani