Biashara nyingi katika kivuko cha Likoni Feri kaunti ya Mombasa zimetajwa kuathirika pakubwa kutokana na mvua kubwa iliokua ikinyesha.
Kulingana na wanabiasha wa eneo hilo bidhaa nyingi zimeharibika kutokana na mvua hiyo kwani wanabiashara hao walishindwa kufungua wakati kukinyesha.
Wakizungumza na meza yetu ya biashara wanabiashara hao wameeleza kuwa kivuko cha feri ni sehemu maarufu kwa biashara mbalimbali hivyo basi kuna haja ya eneo hilo kujengwa soko ili waweze kutekeleza biashara zao nyakati zozote licha ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Abbadlla Ali mmoja wa wanabiashara hao amedokeza kuwa iwapo hakutakua na mikakati ya kudumu ili kuwawezesha kuendeleza biashara zao nyakati za mvua basi hasara kubwa itawakumba kila kunaposhuhudiwa mabadiliko ya hali ya hewa.
Haya yanajiri huku wachuuzi mbalimbali wakiwemo wa vyakula wakishindwa kuhimili mvua iliokua ikinyesha katika eneo hilo.