Mashirika ya kijamii hapa Mombasa yamewasilisha amri ya mahakama kwa ofisi ya gavana wa Mombasa na kwa bunge la kaunti kushinikiza kuundwa kwa sheria itakayofanikisha makongamano ya bajeti.
Wakizungumza na wanahabari baada ya kuziwasilisha nakala hizo, mwenyekiti wa mashirika ya kijamii hapa Mombasa Zedekiah Adika amesema tangu serikali za ugatuzi, bunge la kaunti ya Mombasa limekuwa likipasisha bajeti na sheria mbalimbali bila kufuata taratibu zinazostahiki ikiwemo kuhusisha vikao vya umma.
Kulingana nao pesa zimekuwa zikitumika kinyume na sheria kutokana na ukosefu wa sheria hiyo na walienda mahakamani kushinikiza taratibu hizo kufutwa.
Aidha wanataka taratibu za bajeti ya mwaka wa kifedha 2022/2023 kutoandaliwa iwapo sheria hiyo haijatengengenezwa.
Kitengo hicho kinahusisha wananchi wanaoteuliwa kisheria pamoja na mawaziri wa kaunti.
Mashirika hayo yamesema kuwa iwapo halitatekelezwa watalazimika kurudi mahakamani ili kuona kuwa wahusika wanachukuliwa hatua za kisheria.
Mwandishi: Ibrahim Juma