Zaidi ya wanafunzi 60 kutoka kwa baadhi ya madrasa hapa Mombasa wametuzwa zawadi za kufuzu kwa masomo mbali mbali ya dini.

Akizungumza kwenye hafla za kuwatuza wanafunzi wa madrasa ya Hidayatul Atfaal Muslim na ile ya wasichana ya Markaz Al-Reyhaan hapa Mombasa Mbunge wa Mvita Abdulswadam Shariff Nassir amewataka wazazi kushirikiana na walimu ili kuona kuwa watoto wanapata mafunzo Zaidi ya dini kama njia moja wapo kujenga msingi bora kwa jamii ya siku za usoni.

Kulingana naye walimu wamechangia pakubwa katika kuboresha nidhamu kwa wanafunzi akitaja  ushirikiano baina ya walimu na  wazazi kama mwelekeo bora utakao imarisha dini na kudumisha zaidi nidhamu kwa wanafunzi.