Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini, ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 90.

Rais Cyril Ramaphosa ametangaza tanzia hiyo leo akimtaja Askofu Tutu kama kiongozi aliyekuwa dira ya kimaadili ya nchi hiyo.

Ramaphosa amesema kifo hicho ni ukurasa mwingine wa majonzi kwa taifa hilo wakati likimuaga kiongozi huyo wa kizazi maalum cha ukombozi wa Afrika Kusini.

Tutu alituzwa Tuzo ya Amani ya Nobel kufuatia mapambano yake yasiyo ya vurugu dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi mnamo mwaka 1984.

Hata baada ya kuangushwa kwa utawala wa ubaguzi wa rangi, mpiganiaji uhuru huyo aliendelea na harakati zake akikosoa mapungufu ya tawala za Afrika Kusini na visa vya ukiukwaji wa haki za binaadamu popote duniani.

Yeye ndiye alinzisha neno maarufu la “Rainbow Nation”, yaani taifa la rangi ya upinde wa mvua, akimaanisha Afrika Kusini wakati Nelson Mandela alipokuwa rais wa kwanza mweusi nchini humo.

Kwa hisan ya DW.

Show more post