Urusi yataka kikao cha Baraza la Usalama kuhusu uhalifu wa mjini Bucha
Urusi imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufanya kikao leo Jumatatu, kujadili ilichokiita ''uchokozi wa Waukraine wenye msimamo mkali'' katika mji wa Bucha, baada ya serikali ya Ukraine kuwatuhumu wanajeshi wa Urusi kuuwa raia katika mji huo.