Majeshi ya Ukraine yashambulia daraja la kimkakati litumiwalo na Urusi
Jeshi la Ukraine limefanya mashambulizi katika daraja moja la kimkakati linalotumiwa na Urusi kwa ajili ya kuyambazia majeshi yake yaliyoko kusini mwa nchi hiyo silaha.
Jeshi la Ukraine limefanya mashambulizi katika daraja moja la kimkakati linalotumiwa na Urusi kwa ajili ya kuyambazia majeshi yake yaliyoko kusini mwa nchi hiyo silaha.
Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zimekubaliana juu ya mpango wa dharura wa kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na hatua ya Urusi kusitisha usafirishaji wa gesi.
Korea Kaskazini leo imeishutumu Marekani kwa kutengeneza silaha za kibaiolojia nchini Ukraine na kurejelea madai ya Urusi yaliyopuuziliwa mbali na Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Machi.
Jeshi la China limekuwa tishio na hatari zaidi katika miaka mitano iliyopita, mkuu wa jeshi la Marekani alisema wakati wa ziara yake katika kanda ya Indo-Pacific akianza na ziara hiyo Jumapili nchini Indonesia.
Mamia ya wanajeshi wa Sri Lanka pamoja na polisi mapema Ijumaa wamevamia kambi moja ya waandamanaji wanaoipinga serikali kwenye mji mkuu wa Colombo, wakati wakiharibu mahema ya wanaharakati wanaosemekana kutokuwa na silaha.