Klabu ya Kick Martial Arts kutoka Ukunda ikishirikiana na shirika la ndege la skyward express wataandaa mashindano ya mbio za half marathon iliyopewa jina la “the Kick out Unfitness” itakayoanza kesho jumamosi .

Lengo la mbio hizo ni kusaidia na kuhakikisha kuwa vijana wamekuzwa katika nyanja ya michezo,kuboresha afya zao na kujishughulisha na masuala muhimu katika jamii.

Kulingana na shirika hilo la ndege la Skyward linaamini kwamba vijana ndio viongozi wa siku za usoni,hivyo basi kuna haja ya kukuza na kusaidia vipaji vyao kwa kila njia

Zaidi shirika hilo limesema kwamba ni kutokana na kuongezeka kwa wateja wao huko Diani tangu waanzishe safari zao mwaka wa 2018 na ushirikiano mwema na wakazi wa kaunti ya Kwale ndio maana wanaandaa michezo kama hiyo ili kuregesha shukrani kwa wakazi hao.

Huku wakiwa na matumaini kuwa mashindano hayo ya mbio yataafikia malengo yake na kukua zaidi katika siku zijazo.

Kwenye mechi za raundi ya 16 za ligi ya mabingwa ulaya zilizochezwa Jumanne 23 Februari 2022 Chelsea waliitandika Lille mabao mawili bila jawabu katika uwanja wa Stamford Bridge.

Kai Havertz alitangulia kufungia Chelsea bao la uongozi katika dakika ya tisa ya kipindi cha kwanza kabla ya Christian Pulisic kuongeza bao la pili katika dakika ya 63.

Kwenye mechi nyengine ya raundi ya 16 Villarreal ilitoka sare ya bao moja na Juventus

Dusan Vlahovic aliiweka Juventus kifua mbele katika dakika ya kwanza ya mechi hiyo .

Bao hilo la Dusan limetajwa kuwa la pili lenye kasi zaidi kuwahi kufu.ngwa kwenye ligi ya mabingwa bara ulaya huku pia likiwa bao lake la kwanza kwenye mechi yake ya kwanza akichezea Juventus.

Hatahivyo Villarreal walisawazisha bao hilo katika dakika ya 66 kupitia Dani Parejo

Shirika la ndege la Skyward Express hii leo limeanzisha ligi ya michuano ya soka kwa vijana huko Lodwar.

Mashindano hayo ambayo yamepewa jina la Skyward Express League Curtain Raiser Edition yameanza hii leo na linatarajiwa kukamilika hapo kesho.

Mechi za leo zinazaragazwa katika uwanja wa prisons huko Lodwar.

Kulingana na mkuu wa kituo cha shirika hilo huko Lodwar Abdinasser Mohammed , wameandaa ligi hiyo ili kukuza talanta za vijana hasa upande wa michezo.

Timu zote kutoka kaunti ya Turkana zimeshiriki kwenye mashindano hayo ambapo ni timu 4 za wavulana na 2 za wasichana.

Timu za wanaume ni pamoja na Lodwar Fc, Earthmovers Fc, Hill Side Fc, na Turkana Allstars FC.

Huku timu za wanawake zikijumuisha Turkana Queens na Home Girl Fc.

Klabu ya Bandari FC imeachana na kocha Andre Cassa Mbungo.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari klabu ya Bandari imesema makubaliano ya kuachana na huduma za kocha huyo yamefikiwa kati ya uongozi wa klabu na mkufunzi mkuu, Andre Cassa Mbungo kusitisha kandarasi yake.

Aidha uongozi wa Bandari unamshukuru Cassa Mbungo kwa juhudi zake na mafanikio aliyoyapata akiwa klabuni hapo, yakiwemo kutangazwa kama kocha bora kwa wiki tatu mtawalia na kuibuka katika nafasi ya tatu kwa kitengo cha kocha bora, msimu uliopita.

Hata hivyo, matokeo ya hivi karibuni hayajafikia matarajio ya Bandari msimu huu.

Ligi ya mabingwa bara ulaya iliingia raundi ya 16 bora jana usiku ambapo kulichezwa mechi mbili.

PSG waliokuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa parc de princes waliibuka na ushindi mwembamba wa bao moja dhidi ya Real Madrid.

Kylian Mbappe alifungia PSG bao hilo la pekee na la ushindi katika dakika za nyongeza.

Kwenye mechi nyengine Manchester City waliifyeka Sporting CP mabao matano bila jawabu.

Ikumbukwe kwamba katika historia hii ni mara ya kwanza kwa shirikisho la soka barani ulaya UEFA kuondoa sheria ya mabao ya ugenini kumaanisha mshindi wa kuingia robo fainali baada ya mikondo miwili atabainika kwa jumla ya magoli waliyofunga au wakitishona kwa magoli basi mshindi atabainika kupitia dakika 30 za muda wa ziada na ikiwa bado timu zitakuwa sare basi mshindi ataamuliwa kupitia mikwaju ya penati.

Pia ni mara ya kwanza ndani ya miaka 18 ,miamba wa Uhispania Barcelona hawamo katika raundi ya 16 ya ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika kundi F na watacheza mchujo dhidi ya Napoli kuwania nafasi ya kushiriki kombe la Europa league awamu ya 16 bora.

Kwenye mechi zengine za raundi ya 16 zitakazopigwa leo RB Salzburg watapepetana na Bayern Munich saa tano usiku.

Nao Inter Milan watakuwa mwenyeji wa Liverpool katika uwanja wa San Siro saa tano usiku.

Show more post

 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani