Manchester City wametinga kwenye nusu fainali ya ligi bingwa ulaya na watavaana na miamba wa Uhispania Real Madrid baada ya kuibandua Atletico Madrid katika mtangange wa robo fainali.

Katika mechi yao ya mkondo wa pili iliyopigwa uwanjani Wenda Metropolitano jana hao Man City walitoka sare tasa na Atletico Madrid.

Man City walipata ushindi wa bao 1-0 kwenye mechi yao ya awamu ya kwanza iliyochezwa wiki iliyopita uwanjani Etihad, na walihitaji sare ya aina yoyote ili kutinga nusu fainali.

Atletico aidha walimaliza mechi hiyo wakiwa wachezaji kumi uwanjani baada ya Felipe kuonyeshwa kadi nyekundu.

Kwenye mechi nyengine Liverpool ilitinga nusu fainali ya ligi bingwa ulaya licha ya kutoka sare ya 3-3 dhidi ya Benfica kwenye ngarambe ya robo fainali iliyogaragazwa uwanjani Anfield jana usiku.

Liverpool walijikatia tiketi ya nusu fainali baada ya kuibuka na ushindi wa 3-1 wiki iliyopita huko Ureno .

 

Beki wa Chelsea Antonio Rudiger anatarajiwa kujiunga na Real Madrid baada ya kukamilisha vipimo vyote vya matibabu. Rudiger amekubali kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bure baada ya kukataa nafasi ya kusalia Chelsea msimu huu.

Beki huyo mjerumani anatarajiwa kujiunga na Real Madrid mwezi julai tarehe moja kwa mkataba wa miaka minne. Inaaminika kuwa mkataba huo una thamani ya yuro laki nne akitia mfukoni yuro laki mbili elfu arobaini na mbili kwa wiki.

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel mwezi uliopita alithibitisha kwamba Rudiger hatosaini mkataba mwengine na klabu hiyo. Klabu kadhaa kutoka ulaya ikiwemo Barcelona, PSG, na Manchester United zilivutiwa na huduma za beki huyo mjerumani.

Aidha beki huyo mwenye umri wa miaka 29 alivutiwa na Real Madrid na sasa ataelekea katika jiji la Uhispania.

Show more post

 

More Stories

Miraa na Mgoka kupigwa marufuku Mombasa

Wanafunzi kurudi shuleni juma lijalo

Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto Pwani