Manchester City walimiliki mechi yao yar obo fainali ya ligi bingwa ulaya awamu ya kwanza baada ya kuitandika Bayern Munich mabao 3-0 katika uwanja wa Etihad.

Rodri alitangulia kufungia City bao la uongozi katrika dakika ya 27 kabla ya Bernando Silva kuongeza la pili katika dakika ya 70 ya kipindi cha pili.

Halaand alifunga hesabu ya mabao matatu baada ya kufungia City bao la tatu katika dakika ya 76.

Mechi ya marudiano itagarazwa Munich aprili 19 lakini hao city wanakabiliana na Leicester City kwenye ligi ya primia uwanjani Etihad Jumamosi wikendi hii.

Bunrley waliibuka na ushindi wamabao 2-1 dhidi ya Middlesbrough sikuya ijumaa kwenye mechi yao ya ligi ya championship huku ushindi huo ukiwarejesha tena kwenye ligi ya primia Uingereza.

Burnley inmayofunzwa na mchezaji wa zamni wa Man city Vincent Kompany imekua moto wa kuotea mbali msimu huu na wamekuwa kileleni mw aligi hiyo tangu mwezi oktoba.

Lejendari huyo wa Manchester City ameongoza klabu hiyo hadi kurejea kwenye ligi ya primia kwa mara ya kwanza akiwa kocha mchanga mwerevu kwenye soka ya uingereza.

Huku Kompany akiongoza klabu hiyo msimu ujao, Burnley wanaweza kuwa na matarajio tofauti sana na walivyokuwa hapo awali kwenye Premier League.

Burnley wamepoteza mechi mbili pekee na wanaongoza ligi kwa kuweka mwanya wa alama 11 mbele ya Sheffield United .

Kompany kwa sasa anahitaji ushindi zaidi ili kupata medali yake ya kwanza akiwa kocha huku klabu kubwa za uingereza zikivutiwa na kocha huyo mbelgiji.

Mwanariadha Grace Wanjiru ameshindia Kenya medali ya tatu ya dhahabu kwenye Riadha za Dunia za Ukumbini za watimkaji wanaozidi umri wa miaka 35 mjini Torun, Poland, Jumanne.

Wanjiru ambaye ni bingwa mara sita wa bara afrika aliwapiku wapinzani wenzake vumbi katika fani ya matembezi ya haraka ya mita 3,000 uwanjani Arena Torun, siku moja baada ya Erick Sikuku na Kenneth Mburu kubeba mataji ya matembezi ya haraka ya 3,000m na mbio za nyika za kilomita nane katika washiriki walio na umri kati ya miaka 45 na 49 mtawalia.

Rebecca Mulatya alijishindia nishani ya fedha ya kuruka umbali (Long Jump) siku ya Jumatatu kwa upande wa kinadada walio kati ya umri wa miaka 45 na 49.

Siku ya Jumanne, mwanaolimpiki Wanjiru alitamba katika kitengo chake cha wanawake walio kati ya miaka 40 na 44 baada ya kutwaa taji kwa muda wake bora msimu huu, dakika 14 na sekunde 15.19.

Kenya inawakilishwa na wanariadha 18 katika mashindano hayo ya kila baada ya miaka miwili yaliyoanza Aprili 26.

Kwa sasa, Kenya iko katika nafasi ya 20 ikiwa na dhahabu tatu na fedha moja. Ujerumani imekaa juu ya jedwali kwa medali 95 (dhahabu 31, fedha 30 na shaba 34) ikifuatiwa na Poland (dhahabu 30, fedha 29 na shaba 18) na Amerika (dhahabu 16, fedha 18 na shaba saba).

Tunisia ni ya pili barani Afrika na 31 duniani kwa dhahabu moja, fedha moja na shaba moja.

 

Idara ya michezo kaunti ya Lamu imesitisha shughuli za michezo hadi pale mwezi mtukufu wa Ramadhan utakapokamilika.

Mkurugenzi wa michezo kaunti ya Lamu Peter Ndichu amesema wametoa nafasi hiyo ili waislamu makini katika ibada zao na kisha baada ya Ramadhani ratiba za michezo zitarudi kama kawaida.

Amesema kutokana na utukufu wa mwezi wa Ramadhani kwa waumini wa kiisilamu idara ya michezo iliamua kusitisha shughuli zake kwa muda kama njia ya kuonyesha heshima kwa mambo ya ibada ikizingatiwa kuwa asilimia kubwa ya wakaazi wa Lamu ni Waisilamu.

Aidha amesema vijana waliotumbukia katika utumizi wa mihadarati wanapaswa kutumia Ramadhani kama fursa ya kujitoa katika uovu.

Amesema kama mtu anaweza kujizuia kutumia uraibu kwa mwezi mzima hii inaashiria kuwa mtu anaweza kuwacha kabisa uraibu baada ya Ramadhani endapo ataamua.

 

Timu ya soka ya shule ya upili ya wavulana wa Serani ndio washindi wa mkoa wa pwani kwenye michezo ya shule za upili baada ya kuichapa shule ya upili ya kinondo kutoka Kwale mabao 4-3 kupitia mikwaju ya penalti  baada ya kutoka sare ya bao moja  katika muda wa dakika 90 kwenye uwanja wa taasisi ya mafunzo ya walimu Shanzu leo jumamosi.

Kwenye safari yao ya kuelekea fainali Serani waliibuka na ushindi wa mabao matau dhidi ya shule ya upili ya Kenyatta katika ngarambe ya nusu fainali.

Ikumbukwe kwamba Serani ni mabingwa wa kenya na washindi wa pili bara afrika kwenye mashindano ya copa coca cola.

Show more post