Uwanja wa Royal Golf Club kaunti ya Nairobi utakua mwenyeji wa mashindano ya Safaricom Golf Tour mkondo wa 14.
Michuano hiyo ya wikendi ambayo ni ya mwisho kabla ya fainali zitakazopigwa wiki ijayo huko Vipingo Ridge, imevutia zaidi ya washiriki 350 .
Michuano hiyo ya kishirika imeratibiwa kufanyika jumamosi huku ile ya chipukizi ikifanyika jumapili.
Kulingana na mkurugenzi mkuu Peter Ndegwa anafurahia hatua walizopiga za kutambua wachezaji wadogo wenye talanta miongoni mwa chipukizi.
Ndegwa ameeleza kuwa wamehusisha zaidi ya washiriki 8, 000 kupitia michuano hiyo, hamasa, na mafunzo ya mchezo huo wa golf uyaliyojumuisha chipukizi 5, 000.
Wikendi iliyopita Nelson Nyoike aliwagaragaza wachezaji golf 253 na kushinda taji la awamu ya 13 uwanjani Vet Lab Golf Club.
Belinda Wanjiru wa miaka 12 na Beiju Shah wa miaka 16 walitawazwa washindi kwenye michuano ya chipukizi baada ya kuwabwaga wachezaji 165 katika uchanjaa huo wa Vet Lab Golf Club .
Michuano hiyo ya wikendi itajumuisha mashindano ya kishirika siku ya jumamosi pamoja na mpango wa uhamasisho unaofahamika kama “Golf Mataani”, ambapo wachezaji wachanga kutoka jamii jirani watapata nafasi ya kujifunza kuhusu mchezo huo wa golf.
Safaricom imewekeza shilingi milioni 100 katika Makala ya uzinduzi wa ziara hiyo kwa lengo la kukuza talanta ya gofu.
Safaricom Golf Tour imefanyika katika viwanja 13 vya golf humu nchini ikiwemo viwanja vya Nanyuki, Limuru, Muthaiga, Nyanza, Machakos, Eldoret, Keren, Nyali, Kericho, Kitale, Nakuru, Kenya Airforce na Vetlab.
Ziara hiyo ya mchezo wa golf itatamatika Vipingo Ridge kaunti ya Kilifi ambako kutapigwa fainali ambapo washindi kutoka kila awamu watapigania tuzo kuu.