Robert Lewandowski ameweka rekodi mpya kwenye ligi ya mabingwa ulaya baada ya Bayern Munich kuicharaza RB Salzburg Mabao 7-1 na kutinga robo fainali.

Lewandowski alipachika hat trick katika mda wa usiopungua dakika 30 na kuweka rekodi mpya kwenye ligi bingwa ulaya.

Munich waliingia kwenye mechi hiyo ya jana wakiwa wametoshana nguvu ya sara ya bao moja kwenye mechi yao ya mkondo wa kwanza.

Lewandowski aliwapa Bayern bao la uongozi katika dakika ya 12 kupitia mkwaju wa penalty.

Dakika tisa baadaye Lewandowski aliongeza bao la pili kabla ya kupachika bao la tatu ndani ya sekunde 120.

Lewandowski mwenye umri wa miaka 33 alichukua dakika 23 kuvunja rekodi ya Marco Simone ya kufunga mabao matatu ndani ya dakika 24 mwaka 1994 akipigia Milan dhidi ya Rosenborg.

Lewandowski sasa ana mabao 12 bao moja mbele ya Sebastien Haller wa Ajax.

Liverpool walionja kufungwa katika uwanja wao wa nyumbani kwa mara ya kwanza ndani yam waka mmoja baada ya kuchapwa bao moja bila jawabu na Inter Milan katika mechi yao ya ligi bingwa ulaya iliyopigwa jana usiku.

Hao Liverpool waliikaribisha Milan wakiwa kifua mbele na ushindi wa mabao mawili bila kwenye mechi yao ya mkondo wa kwanza lakini hapo jana wakapata kipigo cha bao moja huku wakitinga robo fainali.

Lautaro Martinez alifungia Inter bao hilo la pekee huku wakimaliza mechi hiyo wakiwa wachezaji kumi uwanjani baada ya Alexis Sanchez kuinyeshwa kadi nyekundi.

Akiongea baada ya mechi hiyo kocha Jurgen Klopp amekiri kuwa walizidiwa kimhezo na klabu hiyo ya italia licha ya kuwa walitinga robo fainali.
Na kwenye mechi za leo Real Madrid watavaana na PSG kwenye mechi yao ya mkondo wa pili.

Mechi yao ya awamu ya kwanza Real Madrid walifungwa bao moja na PSG.

Nao Manchester City watakabiliana na Sporting Lisbon.

Mechi zote mbili zitaanza saa mbili.

Mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa ulaya Chelsea wamepangwa kumenyana na miamba wa Uhispania Real madrid kwenye robo fainali ya ligi hiyo bingwa ulaya.

Atletico madrid waliowabandua Manchester United watakuwa na safari nyengine ya kuelekea jiji la Manchester kumenyana na Manchester City.

Liverpool angalau wamepata afueni baada ya kupangwa na Benfica huku Bayern Munich wakiratibiwa kucheza na Villarreal.
Villarreal waliibandua Juventus kwenye raundi ya 16, huku Benfica wakiiondoa Ajax.

Wakati uo huo droo ya nusu fainali imetolewa kabisa ambapo Manchester City na Atletico Madrid ,Chelsea na Real Madrid huenda zikakutana kwenye nusu fainali.

Vilevile Benfica au LIVERPOOL , Villarreal na Bayern Munich huenda zikamenyena kwenye nusu fainali hiyo.

Tarehe ya mechi hizo za robo fainali na nusu fainali zitatolewa baadaye.

 

Kocha wa klabu ya Shimanzi Youth FC Nelson Wanjala anasisitiza kuwa kikosi chake kiko tayari kwa ligi ya FKF eneo la pwani .

Kocha huyo amefichua kuwa amevutiwa na utayari wa wachezaji wake ambao wako fiti huku akiamini kuwa wataboresha zaidi mchezo wao msimu huu.

Wanjala ameeleza kuwa wamecheza mechi kadhaa za kujipa nguvu pamoja na kuwapima wachezaji wao wapya .

Wachezaji wapya katika timu hiyo ni makipa Seth Njane, Samuel Okello na washambuliaji Mohammed Abdul na Jacob Karisa wote wakiwa ni wanafunzi wa shule.

Hata hivyo klabu hiyo itakosa huduma za kiungo Bilal Mohammed aliyejiunga na klabu ya ligi ya daraja la pili Kenya Navy.

Sudi Matano aidha ataziba pengo la Bilal Mohammed kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Show more post