Wanaotekeleza biashara kandokando mwa barabara washauriwa kuhama kaunti ya Kwale.
Waziri wa utalii na biashara kaunti ya Kwale Michael Mutua amewataka wafanyibiashara wa Ukunda wanaohudumu kando kando mwa barabara kuhamia katika soko jipya lililojengwa na serikali ya kaunti hiyo.
Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa soko hilo, Mutua ameagiza kusikitishwa kwa shughuli zote za kibiashara zinazoendelezwa kando ya barabara kuu ya Likoni - Lungalunga kwa usalama wa wafanyibiashara hao.
Kauli ya waziri huyo inajiri baada ya baadhi ya wafanyibiashara wa soko la Ibiza na Kalipso kudinda kuhamia katika soko jipya la kaunti lililoko eneo la Mvindeni.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyibiashara waliohamia katika soko hilo wamewarai wenzao kujiunga nao ili kuendeleza shughuli zao pamoja.
Wakiongozwa na Juma Malombe, wafanyibiashara hao wameelezea kuridhishwa kwao na jinsi hali ya usalama imeimarishwa katika soko hilo.