Mbunge wa Kinango Gonzi Rai amezindua ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya Msingi ya Bumburi eneo hilo la Kinango kaunti ya Kwale.
Kulingana na mbunge huyo ujenzi huo wa madarasa mawili utagharimu takriban shilingi milioni 2.8 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Gonzi amesema kuwa ujenzi wa madarasa hayo utafaidi zaidi ya wanafunzi 90 akiongeza kuwa mradi huo ni miongoni mwa mikakati yake ya kumaliza tatizo la uhaba wa madarasa katika shule hiyo pamoja na kuimarisha viwango vya elimu katika eneo hilo la Kinango.
Mradi sawia na huyo unaendelea katika shule ya msingi ya Kajiweni central wadi ya Mackinon.