Hatimaye muungano wa mabaharia nchini SUK waandaa uchaguzi wake

Hatimae Muungano wa mabaharia nchini SUK umeandaa uchaguzi wake rasmi katika ukumbi wa Licodep eneo bunge la Likoni kama ilivyoratibiwa baada ya uamuzi wa mahakama ya leba.Katika uchaguzi huo,...

Kongamano la kujadili uchumi wa baharini lakamilika huku hamasisho zaidi zikitolewa kupiga jeki juhudi hizo

Kongamano la kujadili mbinu za kuboresha uchumi wa baharini baina ya mataifa wanachama wa IGAD limekamilika rasmi hapa jijini Mombasa.Kongamano hilo la siku nne liliwaleta pamoja wawakilishi kutoka...

Buriani jenerali Francis Ogolla

Seneta Miraj amtetea waziri wa afya

Bandari ya Lamu kuipiku ile ya Mombasa asema Mbogo

Mwenye kiti wa mradi wa LAPSSET Ali Mbogo amesema kuwa bandari ya Lamu inao uwezo wa kuipiku ile ya Mombasa ki biashara ndani ya siku chache zijazo.

Mbogo amesema kuwa baada ya mipango yote kukamilika, meli nyingi za zitakuwa zinatia nanga katika bandari ya Lamu na hivyo basi kuimarisha uchumi wa kaunti hio.
"LAPSSET ni kiungo muhimu katika jamuhuri ya Kenya hivi tunavyozungumza kwa sababu LAPSSET itakapokuwa imetimiza malengo yake basi itafungua asilimia 70 ya jamuhuri ya Kenya" Amesema Mbogo

Akizungumza na mwanahabari wetu, Mbogo amesema kuwa serikali imekuwa na mikutano na washirika wake katika mradi wa LAPSSET yani Ethiopia na Sudan Kusini ili kuona kuwa meli nyingi za kubebea mizigo zinatia nanga katika bandari ya Lamu.

Kutokana na mikutano na mashauriano kati ya Kenya na washirika hao, hivi karibuni Ethiopia itakuwa inapokea meli yake ya kwanza kupitia bandari ya Lamu itakayokuwa imebeba mbolea ya tani 48.

"Hii si biashara ambayo imetolewa Mombasa na kuletwa Lamu. Hii ni biasha ambayo tumeitoa Djibout kwa sababu walikuwa wakipata huduma kuto taifa hilo. Sasa tumeweza kuwashawishi na tukakubaliana waanze kutumia bandari ya Lamu ambao wao ni washirika wakubwa" Akaongeza Mogo

Vile vile Mbogo amesema kuwa wakaazi wa Lamu na pia kutoka maeneo mengine watafaidika kupitia ajira.

 

 


RadioRahma ads