Wawakilishi wateule watano wenye utata katika bunge la Kwale wamejitetea na kushikilia kuwa wanahudumu katika bunge hilo kufuatia agizo la mahakama wala sio kinyume cha sheria kama inavyodaiwa.

Wakiongozwa na mwakilishi mteule Josphine Kinyanjui anasema kwamba watano hao waliteuliwa ili kuwakilisha makabila madogo kaunti ya Kwale kwa mjibu wa sheria za kikatiba.

Hata hivyo amehoji kuwa wako na haki yakutekeleza majukumu bungeni humo kama wawakilishi wadi wengine hivyo kutaka swala hilo kutotiliwa siasa za ukabila hadi pale mahakama itakapotoa uamuzi wa mwisho dhidi ya kesi hio.

Hata hivyo spika wa bunge la Kwale Seth Mwatela Kamanza akishikilia kuwa hana mamlaka ya kuzuia utendakazi wa watano hao hadi pale atakapopata mwelekeo kutoka kwa taasisi husika.