Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amewaomba viongozi wa pwani kuwa na umoja na uwiano na kuhubiri amani ilo kuepuka migogoro inayoshuhudiwa kila mara.

Kauli ya gavana Nassir inajiri baada mgogoro kuibuka katika sherehe iliyohudhuriwa na aliyekuwa waziri wa masuala ya jinsia Aisha Jumwa.

Chimbuko la mgogoro huo ni sherehe ya kimijikenda maarufu chenda chenda iliyofanyika katika Kayafungo Kaloleni kaunti ya Kilifi.

Nassir ametaja umoja wa viongozi wa pwani kama suala bora la kuunganisha wa pwani.

Hata hivyo mgogoro huo ulizuka baada ya wafuasi wa Jumwa kuzua vurugu na kuharibu sherehe hio iliyoandaliwa na gavana Mung'aro.

Fujo hizo zilimsababisha Aisha Jumwa kuondoka mapema katika sherehe hiyo kabla ya kuwahutubia wakaazi hali ambayo gavana Mung'aro aliikashifu.