Gavana wa Kaunti ya Kwale Fatuma Achani amesema serikali yake itaendelea kuboresha Sekta ya kilimo hasa katika maeneo kame.
Achani amesema atafanikisha hilo kupitia uchimbaji wa Mabwawa ili kukabiliana na janga la njaa linalosababishwa na kiangazi katika maeneo hayo.
Kiongozi huyo amesema uchimbaji wa mabwawa 17 katika kaunti hio ikiwemo mabwawa ya Nyalani, Kizingo na Mwaluvuno huko Kinango, kumesaidia kukuza kilimo cha unyunyiziaji katika maeneo hayo, huku ekari zaidi ya 200 zikinufaika na mpango huo wa kilimo.
Kulingana na wakulima wa Kaunti hio wakiongozwa na Ndoro Nyondo, wamesema mpango huo wa uchimbaji mabwawa umewasaidia kuzalisha mazao ya kutosha.
Nyondo amesemahapo awali walilazimika kutegemea chakula cha misaada wakati wa kiangazi.