Mwaniaji wa nafasi ya uwenyekiti wa umoja wa afrika Raila Odinga,ametangaza kuunganisha mataifa ya bara la afrika kufanikisha ustawi wa kiuchumi endapo atapata nafasi hio.
Raila amesema licha ya bara la afrika kuwa na ukwasi wa madini na utamaduni, umaskini,njaa,vita,ukosefu wa ajira na maradhi,imesalia kuwa kizingizi cha maendeleo.
Odinga ameahidi kutumia nafasi yake ya uwenyekiti,kufanikisha ripoti mbali mbali za umoja wa afrika ili kuafiki malengo ya ustawi kwa haraka.

Kiongozi huyo amefichua kua ripoti ya hivi punde ya benki kuu ya afrika inaorodhesha bara la afrika kuwa katika nafasi ya pili kiustawi baada ya bara la Asia.
Odinga ameahidi chini ya uwenyekiti wake, ataghuisha uchumi wa bara la afrika kwa kutoa visa ya AU ambayo itampa fursa mwananchi wa bara hili kuingia nchi yoyote bila vikwazo.

Kwa upande wake rais William ruto amemsifia Odinga na kumtaja kama kiongozi shupavu na alie Nn ufahamu wa kutosha kuhusu bara la afrika na dunia nzima.

Waziri huyo mkuu wa zamani atakabiliana na Mohamoud Youssouf wa Djibouti Anil Gayan wa Mauritius na Richard Randriamandrato wa Madagascar, kuwania wadhifa huo.