Serikali ya kaunti ya Mombasa imetoa amri kwa idara ya zimamoto pamoja na wizara ya elimu Mombasa kufanya ugakuzi katika shule zote zilizopo kaunti ya Mombasa ili kubaini endapo Kuna hatari yoyote ya kuibuka kwa Mikasa ya moto.

Akizungumza hapa Mombasa, gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ameviamrisha vitengo hivyo viwili kuandaa mafunzo msingi ya usalama kwa wanafunzi na walimu katika shule mbali mbali kama njia Moja wapo ya kujikinga endapo kutatokea dharura ya moto shuleni.

Hatua ya gavana Nassir inajiri siku chache tu baada ya kuibuka kwa mkasa wa moto ulioteketeza bweni katika shule ya Hillside Endarasha kaunti ya Nyeri na kusababisha Vifo vya wanafunzi 18.

Vile vile Nassir ameagiza shule zote za chekechea za kaunti ya Mombasa kuwekwa vifaa vya kudhibiti majanga.

Aidha ameitaka serikali ya kitaifa kupitia hazina ya NG-CDF kuwekeza katika utayarifu wa mashule wa kupambana na dharura yeyote.