Hasmukh Patel, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mombasa Cement ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 58.
Patel, ameaga dunia alipokuwa akikimbizwa katika hospitali ya kibinafsi huko Nyali.
Mwakilishi wadi wa Tudor Samir Bhalo, ambaye pia ni mtu wa karibu wa familia, amethibitisha kifo cha Patel.
Mwili wa mfanyabiashara huyo umehamishiwa katika makafani ya Hospitali ya Pandya Memorial, Mombasa.
Patel alijulikana kwa kuendesha miradi kadhaa ya hisani katika kaunti za Mombasa, Kilifi na Kwale.

Patel anadaiwa kuhisi maumivu ya tumbo akiwa nyumbani kwake alipofariki.
Patel amekuwa akiendesha miradi kadhaa ya kusaidia jamii ikiwemo kuwalisha yatima na vijana wa mitaani.
Miongoni mwa waliomwomboleza Patel ni Gavana wa kaunti ya Mombasaa Abdulswamad Nassir, aliyemtaja kuwa mkarimu na mshirika wa karibu kwa uongozi wa kaunti ya Mombasa.