Mwili wa mwanamume mmoja umeopolewa huku juhudi za kuusaka mwili wa pili zikiendelea baada ya boti lililokuwa limebeba watu sita kupinduka katika bahari hindi eneo la Kinondo huko Msambweni kaunti ya Kwale usiku wa kuamkia leo.

Watu hao wanaokisiwa kuwa wavuvi walikuwa wakielekea eneo la Shimoni huko Lungalunga kutoka kaunti ya Mombasa .

Akithibitisha tukio hilo naibu kamishna eneo la Msambweni Josphat Musyoki amesema kwamba juhudi za wapiga mbizi kutoka kwa kikosi cha walinzi wa Pwani yani Kenya coast guard, polisi na maafisa wa msalaba mwekundu za kuusaka mwili wa pili zinazidi kutatizika kufuatia makali ya mawimbi.

Mwili wa mwendazake Stephen Odhiambo mwenye umri wa miaka 44 unahifadhiwa katika mochari ya hospitali ya rufaa ya Msambweni huku juhudi za kuusaka mwili wa Haji zikiendelea.