Mkurugenzi wa mauzo katika kiwanda Cha Revital kilichoko kaunti ya Kilifi Roneek Vora amesema kuwa kiwanda hicho kinaendelea kuweka mikakati kabambe ili kukabiliana na ugonjwa wa Mpox.
Kwa mujibu wa Roneek Vora kiwanda hicho kinalenga kushirikiana na mataifa ya bara Afrika ili kuzisambazia vifaa vya matibabu hasa wakati huu ambapo mataifa mengi yanakodolea macho mkurupuko wa ugonjwa wa Mpox
Wakati uo huo ametoa wito Kwa viwanda vinavyopatikana humu nchini kuajiri watu wanaoishi na ulevu iliwaweze kujikimu kimaisha.
Vora amesema kuwa wanatarajia kufungua kiwanda kikubwa Ndogo kundu kitakachowezesha kutoa ajira zaidi humu nchini na kurahisisha kupatikaniwa Kwa vifaa vya upimaji maradhi mbalimbali ili wagonjwa wapate tiba Kwa wakati unao stahili.
Kwa upande wake mshirikishi wa mipango katika chama cha wahariri Ken Bosire ametoa wito wa kuunga mkono uzalishaji unaoptikana humu nchini.