Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa chanjo dhidi ya virusi vya corona iliyotengenezwa na kampuni ya Moderna inaweza kutumika kwa dharura, na kuwa chanjo ya tano miongoni mwa zilizoidhinishwa na shirika hilo ili kutumika na mataifa ulimwenguni.
WHO imesema lengo la hatua hiyo ni kuwezesha upatikanaji wa haraka wa dawa, chanjo na vifaa vya uchunguzi kukabiliana na dharura iliyopo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Mariangela Simao, alisema kwamba sasa ni muhimu kuwa aina nyingi za chanjo baada ya kujitokeza kwa changamoto ya usambazaji wake ikiwemo kutoka India, taifa ambalo linakabiliwa na wimbi kubwa la maambukizo ya Covid- 19.
Mbali ya chanjo ya Moderna, WHO pia tayari ilitoa ithibati kwa chanjo za Pfizer, AstraZeneca, Johnson & Johnson na nyingine iliyotengenezwa na taasisi moja ya India.
Kwa Hissani ya DW SWAHILI