Watu 427 wamepatikana na virusi vya corona ,kutoka sampuli 3,307 zilizopimwa saa 24 zilizopita.

Kiwango cha maambukizi humu nchini kimefikia asilimia 12.9Kutokana na visa hivyo 396 ni wakenya na 58 ni raia wa kigeni.
221 ni wanawake na 206 ni wanaume.

Mgonjwa mwenye umri mdogo ana mwaka mmoja na mwenye umri mkubwa ana miaka 92.

Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa jumla ya visa 225, Kiambu 73, kitui 33, Kilifi na Siaya visa 21, Nakuru 13, Mombasa na Murang’a visa 8, Uasin gishu 6, Nyeri na Tana River visa 3, Kericho, Laikipia, Lamu, Makueni na Turkana visa 2, Machakos, Meru na Nyandarua kisa kimoja kila kaunti.


Wagonjwa 80 wamepona ugonjwa huo wote kutoka kwa mpango wa kutengwa na huduma ya nyumbani.Hakuna mgonjwa aliefariki, hivyo basi idadi ya waliofariki kutokana na virusi hivyo ikibakia 5,651.

Wagonjwa 47 wako katika vituo mbalimbali vya afya humu nchini huku 3,065 wako katika mpango wa kutengwa na huduma ya nyumbani.