Gavana mteule wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amewatembelea wakaazi wa Kibarani hapa Mombasa.

Nassir ametoa hakikisho kwa wakaazi wa eneo hilo kwamba ahadi alizozitoa wakati akitafuta nyadhfa ya ugavana, atazitekeleza pindi atakapo apishwa rasmi kama gavana wa Mombasa.

Nassir ambaye alikuwa ameandamana na mbunge mteule wa eneo la Jomvu Badi Twalib amesema miongoni mwa masuala aliyoyapa kipao mbele pindi tu atakapoapishwa ni ikiwemo kuangalia suala la ajira kwa vijana na wakaazi wa kaunti ya Mombasa.

Kwa upande wake mbunge mteule wa Jomvu Badi Twalib amewashukuru wakaazi wa eneo bunge hilo kwa kumchagua Nassir kuwa gavana wa pili akiwahakikishia kwamba mataqwa yao yatatekelezwa.Nassir anatarajiwa kuapishwa tarehe 15 Septemba mwaka huu.