Vijana katika kaunti ya Kwale wameonywa dhidi ya kutumika na wanasiasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Agosti.

Mgombea wa kiti cha ugavana wa kaunti hiyo Prof. Hamadi Boga amewataka vijana kutotumika vibaya kuzua vurugu wakati huu wa msimu wa siasa.

Akizungumza katika eneo la Diani, Boga amesema kwamba vurugu hizo zinalenga kuwaathiri vijana na jamii kwa ujumla.

Kauli yake imeungwa mkono na afisa wa shirika la kijamii la Kenya Community Support Centre KECOSCE Vivian Muge aliyewataka vijana kudumisha amani.

Muge amesema kuwa tayari shirika hilo linaendeleza mpango wa kuhubiri amani wakati huu wa msimu wa siasa katika jamii.