Jumla ya watu 125 wamefaidika kutokana na waqfu wa One Shilling Foundation katika kaunti ya Mombasa.

Kulingana na mwanachama wa waqfu huo Sheikh Abuu Hamza, Miongoni mwa walionufaika ni wanafunzi waliomaliza darasa la nane ambao wataweza kulipwa karo zao katika shule za upili, pamoja na kina mama wasiojiweza kwenye jamii ambao wamepewa cherehani pamoja na vyombo vya kujianzishia biasahara ili wajikimu kimaisha.

Abuu Hamza amesema kwamba kila mwaka takriban wanafunzi 500 ambao humaliza kidato cha nne hunufaika kutokana na waqfu huo kwa masomo ya tarakilishi huku walengwa wakiwa mayatima na vijana kutoka jamii zisizojiweza.

Sheikh Abu Hamza aidha amesema kwamba mradi huo wameipa kipaumbele sekta ya elimu ili kuweza kusaidia katika kuwenusha hali ya elimu kwa wakaazi wa ukanda huo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa hazina ya ustawi wa eneo bunge la Mvita (CDF) Omar Shariff akimuwakilisha mbunge wa Mvita Abdulswammad Shariff Nassir, amesema kwamba waqfu huo umechangia pakubwa kuyaenua maisha ya jamii zisizojiweza 

Aidha Shariff ametaka jamii kujitolea na kusaidiana waqfu huo kufanikisha malengo hayo ili kuwezesha wanafunzi wamepata elimu pamoja na kina mama wenye malengo ya kuanzisha biashara zao wamewezeshwa.

Mwandishi: Ibrahim Juma Mudibo.