Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko amenyimwa kibali cha kuwania kiti cha ugavana wa Mombasa.

Tume ya IEBC imetaja kuondolewa kwake madarakani akiwa Gavana wa Nairobi kama sababu iliyomfanya asipewe kibali cha kuwania ugavana.

Wakati uo huo, IEBC ilifahamisha gavana Sonko kwamba hangeweza kuidhinishwa kwa vile shahada yake haikuwa imeidhinishwa na Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu.

Hatua hio ilizua taharuki katika afisi za IEBC huku gavana huyo wa zamani akijaribu kusistiza kuidhinishwa.

Mgombea huyo wa ugavana alikuwa amefika katika Shule ya mafunzo ya Serikali ya Kenya (KSG) ili kuidhinishwa.

Sonko anakodolea macho kiti cha ugavana wa Mombasa kwa tiketi ya Wiper Party.

Aliandamana na mgombea mwenza wake Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo, aliyekuwa mbunge wa Matuga Chirau Mwakwere.