Mimba za mapema kwa wasichana zimetajwa kuwa miongoni mwa tatizo linalo lemaza ndoto ya elimu.

Haya ni kwa mjibu wa mgombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir.

Akizungumza hapa Mombasa Nassir amesema kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wasichana hapa Pwani wanakosa kuendeleza masomo yao kwa sababu ya mimba za mapema.

Nassir ambaye anagombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa amedokeza kuwa serikali yake itaanzisha mpango wa nafasi ya pili(Second Chance program) kwa wanafunzi wa kike ili kuwawezesha wanafunzi waliopachikwa mimba na kuachwa wanapata nafasi tena ya pili ya kuendeleza masomo yao.

Nassir ametaja mpango huwa ni njia bora ya kufufua ndoto ya wanasichana wa kike waliokuwa wamepoteza matumaini ya kuendeleza elimu yao kwa manufaa ya siku za usoni.