Mwili wa afisa wa Polisi umepatikana umetupwa katika eneo la Kibarani hapa Mombasa.

Akithibthisha kisa hicho kamanda wa polisi eneo bunge la Jomvu Lydia Wanjiru amesikitishwa na mauaji ya afisa wa polisi anayefahamika kama Muhidin Sheikh, huku akiwarai raia kutochukua sheria mikononi mwao na badala yake kupiga ripoti polisi ili kupata usaidizi.

Hatahivyo maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi dhidi ya kifo cha afisa mwenzao ambaye ameuawa jana .

Mwili wa marehemu ulikua na majeraha kichwani huku ikiaminika kuwa ameuwa.

Kwa upande wake mzee wa Mtaa wa eneo la Jomvu ,Alex Mwega ameeleza amepashwa taarifa kuhusu kisa hicho cha mwili huo wa afisa wa polisi uliopatikana katika Mangwe huku mmiliki wa Mangwe hiyo akitiwa nguvuni.